Kwa mujibu wa taarifa ya huduma ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Harakati Nujabaa kwa kutoa tamko hilo ilionyesha msimamo mkali kuhusiana na shambulio la hivi karibuni dhidi ya makao ya Hamas huko Doha.
Katika tamko hili wamesema: “Shambulio la kinyama na la usaliti la Wazayuni na Marekani dhidi ya makao ya Hamas huko Doha, wakati wa mkutano kwa ajili ya mpango wa Marekani ambao Hamas kwa hila ilisukumwa kuingia humo.
Harakati hii katika tamko lake imeongeza kuwa: “Harakati ya Nujabaa kwa mara nyingine tena inasisitiza juu ya msimamo wake thabiti na wa kuwaunga mkono ndugu zake wa damu moja na hatima moja wa Hamas; wale ambao wameshusha chini kujisalimisha na maridhiano na, licha ya jitihada zote, wamechagua njia ya kukabiliana.”
Tamko la Nujaba lilikielezea kitendo hiki kuwa cha woga na likabainisha wazi: “Harakati ya Nujabaa inalilaani vikali na kukikataa kitendo hiki cha woga. Wamewalenga viongozi wa ngazi ya juu wa Hamas katika sehemu ambayo ilikuwa imekusudiwa kuwa chini ya makubaliano na uratibu na Qatar na kwa taarifa ya awali ya Trump, ichunguzwe kwa ulinzi.”
Katika mwendelezo wa tamko hili, likiwaelekea viongozi wa Kiarabu, imesemwa: “Tunawaambia Waarabu waliosalimu amri: Kitendo hiki cha usaliti kiekeni mbele ya macho yenu, nyinyi hamko salama kutokana nacho, na hata kwa kujisalimisha na kwa kufanya uhusiano wa kawaida wa aibu pia hamna hatima nyingine!”
Harakati Nujaba mwishoni, ikiwaandikia viongozi wa Kiarabu, iliandika: “Rudini katika asili na ukoo wenu ikiwa kwa hakika nyinyi ni warabu, na simameni pamoja na Palestina iliyojeruhiwa.
Maoni yako